Rais amewateua mawaziri
wanane wapya pamoja na manaibu watano. Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika
ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue. Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa
waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja
na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa
Anna Tibaijuka. Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo
ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo
imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene Rais
Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo lililorushwa
hewani na runinga ya taifa moja kwa moja. Hii ndio orodha ya mawaziri
walioteuliwa
MAWAZIRI
George Simachawene waziri wa
nishati na madini
Mary Nagu- waziri wa nchi
[afisi ya rais] mahusiano na uratibu
Christopher chiza -waziri
uwezeshaji na uwekezaji
Harisson Mwakyembe[waziri wa
ushirikiano wa afrika mashariki]
William Lukuvi -waziri wa
ardhi nyumba na makaazi
Steven Wasira -waziri wa
kilimo chakula na ushirika
Samwel Sita -waziri wa
uchukuzi
Jenista Muhagama -waziri wa
nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge
MANAIBU WAZIRI
Stephen Masele -naibu waziri
afisi ya makamu wa rais muungano
Angela Kariuki -naibu waziri
wa ardhi nyumba na makaazi
Ummi Mwalimu- naibu waziri wa
katiba na sheria
Anna Kilango naibu waziri wa
elimu na mafunzo ya kiufundi
Charles Mwijage-naibu waziri
wa nishati na madini



