kwanza kabisa Krismasi(pia Noeli) ni sikukuu ambayo Wakristo wengi Tunaadhimisha kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida Wengi Tunasheherekea tarehe 25 Desemba kwa wakristo wa magharibi na tarehe 6 Januari kwa wale wa mashariki Hiyo Ni Kutokana Tofauti Za Kalenda. JINA LAKE Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii. *.Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo. *Pia Noeli inatokana na Utohoaji Wa Neno La Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka lugha ya Kifaransa"noël" . Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa"...... .. Kwanini Sasa Iwe Tar 25 December Wakati Biblia nasema Maria Alipashwa Habari Mwezi Wa Sita?? kwanza itambulikane kwa uwazi kabisa kanisa lina utaratibu wa maadhimisho ya sikukuu mbalimbali za watakatifu katika tarehe tofauti tofauti kutokana na umuhimu wao katika imani pili Mwezi wa sita unaosemwa katika Lk 1:26 Katika biblia sio mwezi June bali ni mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeti, ni mwendelezo wa maelezo kutoka mstari wa 24. Hata hivyo hakuna anayejua kwa uhakika Yesu alizaliwa lini kumbe huu ni utaratibu ni wa kanisa kusherehekea(ad himisho) la christmass kila tar 25 dec.
CHANZO CHA KUSHEHEREKEA Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo haijulikani kwa sababu tamaduni Za Kiyahudi Kwa Nyakati Zile hazikuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa. Lakini baadaye Ukristo uliendelea Kukua katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo kwa upendo wa mungu ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo Mkombozi Wetu . Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi. Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200. Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu ...pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari. Labda kadirio la tarehe ya 25 Desemba pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200. (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa. Hivyo Habari za Krismasi katika Biblia hazipatikani katika kwa sababu zilizotajwa hapa juu. Lakini Kwa Hakika vitabu viwili vya Agano Jipya vina habari za kuzaliwa kwake Yesu, yaani Injili za Mathayo na Luka. Hivyo Ni ajabu kutafuta tarehe ya kuzaliwa Yesu wakati hujui hata tarehe ya kuzaliwa babu yako au baba wa babu Yako. KUHUSISHWA NA SIKUKUU YA KIPAGANI YA WARUMI (Sol Invictus) Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kuchukua nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu"Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika" ). Lakini kumbe mambo yalikwenda kinyume, yaani kwamba Makaisari walianzisha sikukuu hiyo, halafu wakaipanga tarehe ya Krismasi ili kushindana na Ukristo uliokuwa bado chini ya dhuluma ya serikali yao. Aliyeingiza sikukuu ya "Kuzaliwa Jua" ( Mitra) huko Romani Eliogabalus kaisari kuanzia 218hadi222). Baadaye Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273, hatimaye ikahamishiwa tarehe 25 Desemba. Wakati wa Licinius( 308- 324) Kabla Hapo sikukuu hiyo ya warumi ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba.. Kutoka Roma, uliokuwa mji mkuu wa Dola la Roma, sherehe ya 25 Desemba ilienea kote katika Ukristo.
Wakristo Hvyo wengi Tunasheherekea tarehe 25 Desemba( Wakatoliki na sehemu ya Waprotestanti na Waorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katika kalenda Inayotumika Ya Julian Ambayo Iko Nyuma Kwa Siku 11 Lakini Propaganda Hizo Bado Azituzuii Kusherehekea Siku Ya Kuzaliwa Kwa Bwana Na Mwokozi Wetu Yesu Kristo. Wao Wanaposema Kuwa Ni Siku Ya Sherehe Za Jua, Tunapenda Kuwaambia kwetu Jua Si Kitu Chenye Kutumainiwa Zaidi Ya Mungu Na Yesu Kristo Ndiye Mwanga Na Nuru Ya Ulimwengu Kama Anapojidhihiris ha Kupitia YOHANA 8;11 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi NURU YA ULIMWENGU, yeye anifuataye hatakwenda gizani. kamwe, bali atakuwa naNURU YA UZIMA.